THRDC YATEMBELEA TAASISI YA IRDO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 23 June 2022

THRDC YATEMBELEA TAASISI YA IRDO




Meneja Programu wa mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania akiwa katika ziara ya kutembelea wanachama wa Mtandao waliopo kanda ya nyanda za juu kusini kwa mikoa ya Rukwa, Songwe na Mbeya, amepata fursa ya kutembelea shirika la Integrated Rural Development Organization (IRDO) iliyopo halmashauri ya wilaya ya Ileje Mkoani Songwe.


Katika ziara hiyo Meneja programu ameambatana na Mratibu wa kanda ya nyanda za juu kusini, Bw. Gabriel John, afisa mkuu wa dawati la wanachama Bi. Lisa Kagaruki pamoja na afisa habari wa Mtandao Bi. Loveness Muhagazi amekutana kwa mazungumzo na taasisi ya IRDO inayoongozwa na Bw. Simon Mwang'onda.


IRDO imeanzishwa mwaka 1989 kama mradi wa chakula kwa lengo la kupambana na majanga ya njaa (Food production Project) na kusajiliwa rasmi mwaka 2012 na kuwa NGO iliyoitwa Integrated Rural Development Organization kufanya kazi katika mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa, Ruvuma na wilaya zake.


IRDO inafanya kazi katika kuhakikisha inaboresha maisha ya wakazi wa ileje na kujihusisha na kilimo cha kisasa, Ujasiriamali, maswala ya Afya hasa HIV na Lishe. Nje ya maeneo hayo inajihusisha na uchechemuzi katika maeneo ya uwajibikaji na utawala Bora, uhaamasishaji wa sera mbali mbali za Kitaifa na kimataifa zinazolenga kuboresha huduma zitolewazo kwa makundi ya watoto, na walemavu, ijulikanayo kama OVC's (Orphans and Vulnerable people).



Taasisi imefanikiwa kuanzisha vituo 6 vya umwagiliaji kuwasaidia wakulima kufanya kilimo cha kisasa, pamoja na ujenzi wa kituo cha VETA Kuwawezesha vijana wa nje ya shule kujiendeleza katika fani mbali mbali.


Pamoja na Kazi kubwa zinazofanywa na taasisi hii bado inakumbana na changamoto kadha wa kadha ikiwemo;


Miradi ya muda mfupi ambayo mara nyingi ikiisha kunakosekana mwendelezo wa kufuatilia wanufaika wanatumia vipi elimu waliopatiwa kipindi cha mradi katika kuendeleza shughuli zao.


Idadi kubwa ya watu ambapo taasisi inashindwa kuwafikia wahitaji wote kutokana na mahitaji.


IRDO si mwanachama wa THRDC, hivyo imeanza mchakato wa kuwa mwanachama ili iweze kuungana na watetezi wengine wa haki za binadamu zaidi ya 200 nchi nzima katika kufanya shughuli za utetezi wa haki za binadamu kwa pamoja.


THRDC imekabidhi baadhi ya machapisho ya Mtandao kwa taasisi hii Ili iweze kujifunza mambo mbali mbali kuhusu Mtandao, lakini pia kupata miongozo mbali mbali juu ya sheria na taratibu zilizowekwa na serikali zinazosimamia mashirika yasiyo ya kiserikali na namna ya kuendana nazo.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso