TAHADHALI YA BARIDI KALI NA KIPUPWE KWA MIEZI MITATU - TMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 3 June 2022

TAHADHALI YA BARIDI KALI NA KIPUPWE KWA MIEZI MITATU - TMA

Mamlaka ya Hewa Tanzania (TMA) imesema ndani ya miezi mitatu kuanzia Juni hadi Agosti, Tanzania inatarajiwa kukutana na hali ya baridi, kipupwe ambacho kinaweza kusababisha baadhi ya maradhi kwa binadamu na wanyama.


TMA imesema kwa kawaida, miezi ya Juni hadi Agosti, huwa ni kipindi cha baridi na upepo lakini kwa mwaka huu hali hiyo kuna uwezekano kuwa siyo kama ilivyokuwa katika miaka iliyopita.


Mamlaka hiyo imeeleza kuwa katika kipindi hicho kutakuwa na vipindi vya upepo mkali vinatarajiwa kushamiri katika maeneo mengi nchini, ambao unatarajiwa utakaovuma kutoka kusini-mashariki na mashariki (Matlai).


Kutokana na hali hiyo kuna matarajio kutokea kwa baadhi ya athari za magonjwa ya mifugo yanayoambatana na baridi kama vile homa ya mapafu yanaweza kujitokeza lakini pia kunatarajiwa kuwa na vumbi inayoambatana na upepo mkali katika baadhi ya maeneo inatarajiwa kujitokeza na inaweza kuathiri afya ya binadamu na wanyama hasa mafua.


Mamlaka ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali wanaotumia taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao.

CHANZO:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso