NA PAUL KAYANDA-HUHESO BLOG
Kufuatia kifo cha Mzee maarufu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, Paul Ntelya mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Mzalendo Foundation, Khamis Mgeja ameushauri uongozi wa Manispaa ya Kahama kutenga mtaa mmoja ambao utaitwa jina lake kwa ajili ya kumuenzi.
Mgeja amesema kuwa Paul Ntelya ni mwanaharakati aliyepigania haki ya kila mtu na alisimama kidete pale alipoona uwajibikaji wa taasisi za serikali unakiukwa katika ngazi ya jamii na alikuwa mkweli hakumuonea mtu au kiongozi yeyote.
"Niishauri tu halmashauri tusahau yale ya nyuma tugange yajayo na tuondoe tofauti zetu huyu mzee alikuwa maarufu na mtetezi wa watu wote hiyo akipewa mtaa jina lake itakuwa kumbukumbu isiyofutika" amesema Mgeja.
Mwenyekiti huyo wa Taasisi ya Tanzania
Mzalendo Foundanion ameyasema hayo leo Juni 25, 2022 baada ya maziko ya mpendwa
wao yaliyofanyika nyumbani kwao katika kijiji cha Kakebe wilayani
humo huku yakihudhuriwa na mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya
Kahama, Thomas Muyonga na waombolezaji wengine.
Marehemu Paul Ntelya alizaliwa tarehe 30/06/1948 na kufariki tarehe 22/06/2022.
No comments:
Post a Comment