NI SIKU KUMI ZA KUWASAKA WAHAMIAJI HARAMU LOLIONDO-ARUSHA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 22 June 2022

NI SIKU KUMI ZA KUWASAKA WAHAMIAJI HARAMU LOLIONDO-ARUSHA




Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala, ametangaza kuanza kwa oparesheni maalum ya siku kumi kwa ajili ya kuwasaka wahamiaji haramu katika eneo la Loliondo na Ngorongoro mkoani Arusha.


Kamishna Jenerali Anna Makakala amebainisha hayo leo Juni 22, 2022 katika Tarafa ya Loliondo, na kusema kuwa zoezi hilo litaenda sawia na zoezi linaloendelea la uwekaji wa alama za mipaka katika pori Tengefu la Loliondo.


"Nchi yetu imebarikiwa kwa kuwa na maeneo mazuri ambayo yanavutia wahamiaji haramu kufika nchini kwa sababu tofauti, hatutakubali hilo litokee wakati wowote ule," amesema Kamishna Makakala.


Dkt. Makakala amesisitiza kufuatwa kwa sheria za nchi pale wageni wanapotaka kuingia au kutoka nchini, na kwamba Uhamiaji wamejipanga vema kusimamia eneo hilo katika mipaka yote nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso