Mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Doto Biteko wilayani Bukombe mkoani Geita amekutwa amejinyonga chumbani kwake huku chanzo cha kifo hicho kikidaiwa kuwa ni kunyimwa chakula na mama yake wa kambo.
Inadaiwa kuwa mwanafunzi huyo alikuwa ananyimwa chakula mara kwa mara anapotoka shuleni na kutotimiziwa mahitaji yake ya shule na mama yake huyo huku watoto wa mama huyo wakitimiziwa mahitaji yao.
Mwanafunzi huyo alikutwa amejinyonga Jumamosi Juni 4, 2022 kwa kutumia tai yake na mkanda wa kiunoni huku akiwa amevaa sare za shule.
No comments:
Post a Comment