Ofisa mtendaji katika kata moja wilayani Siha mkoani Kilimanjaro na mgambo, wanadaiwa kuwatembezea kipigo wanafunzi wanne na kusababisha kifo cha mmoja wao anayesoma kidato cha pili.
Marehemu ambaye ametajwa kuwa ni Bright Arnold (14) na wanafunzi wenzake watatu wa shule ya sekondari Fuka wilayani Siha, wanadaiwa kupigwa ndani ya ofisi ya mtendaji huyo wa kata wakituhumiwa kuiba viatu.
Taarifa za mashuhuda zinaeleza wanafunzi hao walifungiwa katika ofisi ya mtendaji huyo hadi wananchi walipoingilia kati lakini wakati huo marehemu alikuwa hawezi kutembea na baadaye kupoteza fahamu.
No comments:
Post a Comment