MKUU WA TUME YA KUPAMBANA NA UFISADI ASIMAMISHWA NA RAIS, NAFASI YAKE KUSHIKILIWA NA NAIBU WAKE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 10 June 2022

MKUU WA TUME YA KUPAMBANA NA UFISADI ASIMAMISHWA NA RAIS, NAFASI YAKE KUSHIKILIWA NA NAIBU WAKE


Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amemsimamisha kazi mkuu wa tume ya kupambana na ufisadi nchini humo Busisiwe Mkhwebane huku bunge likijiandaa kwa vikao vilivyocheleweshwa kwa muda mrefu vya kumfungulia mashitaka bungeni.


Mkhwebane aliteuliwa katika wadhifa huo na rais wa zamani Jacob Zuma. Uteuzi wake ulionekana na wengi kama jaribio la kumlinda Zuma dhidi ya madai ya rushwa.


Kwa miaka mingi, amewasilisha na kupoteza mahakamani msururu wa kesi za kupinga ya kushitakiwa bungeni.


Bunge ambalo limetawaliwa na chama cha Ramaphosa cha African National Congress, lilikubaliana mwezi uliopita kuanzisha mchakato wa kumshitaki bungeni.


Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Ramaphosa mapema leo inasema Wakili Busisiwe Mkhwebane ataendelea kusimamishwa kazi hadi mchakato ulioanza kwenye Bunge utakapokamilika na nafasi yake itashikiliwa na naibu wake.


Ofisi hiyo imeongeza kuwa kutokuwepo kwa Mkhwebane ofisini hakutazuwia uchunguzi wowote ambao ulianzishwa naye.


Tangazo hilo limekuja ikiwa ni siku moja tu tangu Mkhwebane aanzishe rasmi uchunguzi juu ya Rais Ramaphosa kuficha wizi uliofanyika kwenye nyumba yake ya shambani mwaka 2020.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso