Mkuu wa Mkoa Shinyanga Sophia Mjema amekipongeza Kikundi cha Kahama Hope Givers kwa kuanzisha Mama lishe na Baba Lishe Programme itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi.
Na Naomi Kidunhu-Huheso Digital
Ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na kikundi hicho katika ofisi zao zilizopo maeneo ya Malunga wilayani kahama Mkoani Shinyanga, ambapo amesema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Samia Suluhu itashirikiana nao ili wafikie malengo.
Mwenyekiti wa Kahama Hope Givers Ndg Simon Job Kassala amemshukru Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa kuwatembelea na kuahidi kuwasaidia ili kuhakikisha lengo lao linafikiwa kwa aslimia kubwa
Kwa upande wao Baadhi ya Mama Lishe na Baba Lishe wametoa wito kwa jamii wajitokeze kwenye fursa mbalimbali zinazokuwa zinajitokeza ili kufikia malengo yao.
Kikundi cha Kahama Hope Givers kimeanzishwa kwa lengo la kuwawezesha na kuwakwamua Mama lishe na Baba Lishe itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Sofia Mjema akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Festo Kiswaga wakiwa kwenye ofisi za Kahama Hope Givers
kushoto Katibu wa Kahama Hope Givers Ibrahim Makasy akiwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga pamoja na mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sofia Mjema.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akiwa anasikiliza mazungumzo ya mkuu wa Mkoa Sofia Mjema na kikundi cha Kahama Hope Givers
pichani ni Mwenyekiti wa Kahama Hope Givers akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Sofia Mjema kwenye ofisi ya Kahama Hope Givers
No comments:
Post a Comment