Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro ameendelea kukemea na kulaani vitendo vya mauaji vinavyotokana na wivu wa mapenzi ambavyo vimekuwa vikitekelezwa na baadhi ya watu kwenye jamii jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi.
IGP Sirro amesema hayo akiwa na eneo la Migori mkoani Iringa wakati akizungumza na wananchi wa eneo hilo.
Kuhusu ajali zinazotokana na Pikipiki IGP Sirro amewataka watumiaji wa vyombo hivyo kufuata kanuni na sheria za usalama barabarani na kuhakikisha wanavaa kofia ngumu.
Kuhusu Panya Road IGP Sirro amesema kuwa, jeshi la Polisi limeendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kudhibiti kundi hilo na kuitaka jamii kuhakikisha inaimarisha maelezi ya familia.
No comments:
Post a Comment