TAARIFA KWA UMMA
WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2022
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), linawaita Vijana waliohitimuelimuyasekondari kidato cha sita kwa mwaka 2022, Kutoka ShulezotezaTanzania Bara kuhudhuria Mafunzo ya JKT kwa MujibuwaSheria.
Sanjari na wito huo, JKT limewapangia makambi watakayokwenda kupatiwa Mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 03 hadi 17 June 2022.
Vijana walioitwa wamepangwa katika kambi za JKTRwamkoma-Mara, JKT Msange - Tabora, JKT Ruvu - Pwani, JKTMpwapwa, naMakutupora JKT Dodoma, JKT Mafinga - Iringa, JKT Mlale-Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba -Tanga, JKT Makuyuni -Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa, na JKT Mtabila- Kigoma,JKT Itaka - Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa - Rukwa, JKT Nachingwea - Lindi na JKT Kibiti- Pwani na Oljoro JKT- Arusha.
Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho(Physical disabilities) waripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopoMlandizi Mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumiawatuwajamii hiyo.
JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo. 1. Bukta ya rangi ya ‘Dark Blue’ yenye mpirakiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefuunaoishiamagotini, isiyo na zipu. 2. T-shirt ya rangi ya kijani (Green Vest) 3. Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue. 4. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari. 5. Soksi ndefu za rangi nyeusi. 6. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoayenyebaridi. 7. Track suit ya rangi ya kijani au blue. 8. Nyaraka zote zinazohitajika katika Udahili waKujiungana Elimu ya Juu, zikiwemo cheti vya Kuzaliwa, Vyeti vyaKuhitimu kidato cha Nne nk 9. Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.
Orodha kamili ya majina ya vijana walioitwa, Makambi ya JKTwaliyopangiwa na maeneo yaliyopo pamoja navifaawanavyotakiwa kwenda navyo, Inapatikana katika tovuti ya JKTambayo ni www.jkt.go.tz
Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, Anawakaribishavijanawote walioitwa ili waweze kujiunga na vijana wenzaokatikakujifunza Uzalendo, Umoja wa kitaifa, Stadi za kazi, Stadi zaMaisha na Utayari wa Kulijenga na Kulitumikia Taifa.
Imetolewana:Kurugenzi ya Habari naUhusiano,Makao Makuu ya JKT
Tarehe 31 May 2022.
No comments:
Post a Comment