Wiziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amevitaka vyuo na taasisi zinazotoa taaluma ya uandishi wa habari kufanya tathmini ya mchango wao katika kukuza na kuendeleza tasnia ya habari.
Amesema tathmini hiyo ambayo inapaswa pia kuhusisha wadau wa habari itasaidia kujua mahitaji ya wanataaluma wanaohitajika kwenye soko.
Nape ameyasema hayo leo Jumatano Juni 29, 2022 wakati akifungua kongamano la maadhimisho ya miaka 60 cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam lililolenga kuangalia mchango wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC).
No comments:
Post a Comment