KUFUATIA kifo cha mwendesha boda boda Hiali Mgina (38) mkazi wa mtaa wa majengo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kilichohusisha ajari ya gari aina ya Noa yenye nambari za usajili T 975 DHH na boda boda eneo la Uwanja wa magufuli mkuu wa Wilaya ya Kahama Festo Kiswaga ameliagiza Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kuanza msako wa kuhakiki leseni zao.
Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake Mkuu huyo wa Wilaya ametoa pole kwa familia ya marehemu huyo kwa kufikwa na msiba huo huku akisisitiza jeshi la polisi kuanza msako mkali ili kupitia upya leseni za madereva wote wanaoendesha vyombo vya moto na kuongeza kuwa ajari hiyo inatokana na uzembe wa dereva wa gari hilo.
Imedaiwa kuwa hatua ya boda boda hao pamoja na wananchi kuteketeza gari hilo kwa moto imekuja baada ya mwenzao aliyefahamika kwa jina la Hiali Mgina kufariki kwa kugongwa na gari hili ambapo inasemekana dereva wa gari hilo alikuwa anaendesha chombo hicho cha moto huku amelewa.
Hata hivyo Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga George Kyando amesema kuwa tukio hilo limetokes Juni 19 majira ya saa nne usiku baada ya dereva wa gari hilo kumgonga mwendesha boda boda huyo.
Marehemu Hiali Mgina ameacha mjane na watoto watatu na mwili wake umesafirishwa kuelekea Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma kwaajili ya mazishi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment