KIAMA KWA WATOROSHA MIFUGO NJE YA NCHI HAKUNA WAKUONEWA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 6 June 2022

KIAMA KWA WATOROSHA MIFUGO NJE YA NCHI HAKUNA WAKUONEWA




Kamanda wa Kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo Tanzania ACP Simon Pasua, ametangaza kiama kwa watoroshaji wa mifugo nje ya nchi na kwamba hakuna yeyote mwenye tabia hiyo atakayeonewa huruma.


ACP Pasua amesema hayo leo Juni 06, 2022, wakati akizungumza na askari wa kikosi hicho Makao Makuu ya Kikosi Cha kuzuia wizi wa mifugo (STPU) Jijini Arusha.


Amesema zipo taarifa za watu wachache wanajihusisha na utoroshaji wa mifugo wa mifugo nje ya nchi, ambapo amesema kikosi hakitomuonea muhali mtu yeyote anayetorosha mifugo.


Mkuu huyo wa kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo Tanzania amewataka watendaji wa kikosi hicho kutojihusisha kwa namna yeyote na watuhumiwa wenye lengo la kutorosha mifugo kwani kwa kufanya hivyo kutapunguza pato la Taifa.


Amewataka wafugaji kote nchini kufuata taratibu za uuzaji wa mifugo yao ili kuongeza pato lao na Taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso