KATIBU MKUU MSAIDIZI WA WHO KUFANYA ZIARA YA SIKU NNE TANZANIA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 28 June 2022

KATIBU MKUU MSAIDIZI WA WHO KUFANYA ZIARA YA SIKU NNE TANZANIA




Na.Catherine Sungura,WAF-Dodoma


Katibu Mkuu Msaidizi na Mratibu Mkuu wa Kimataifa wa mapambano dhidi ya UVIKO-19 kutoka Shirika la Afya duniani (WHO) Dkt. Ted Chaiban anatarajia kuja nchini Tanzania mwanzoni mwa mwezi Julai 2022.


Akizungumza na Waziri wa Afya Mwakilishi Mkazi wa WHO nchini Tanzania Dkt.Zabulon Yoti amesema kuwa Kiongozi huyo anatarajia kuwasili nchini kwa ziara ya siku nne kuanzia tarehe 4 hadi 7 mwezi ujao ambapo atapata nafasi ya kutembekea Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Dodoma.


Amesema lengo la ziara hiyo hapa nchini ni kuhamasisha wananchi kupata chanjo ya UVIKO-19 pamoja na masuala mengine ya Afya.


Wizara ya Afya hivi karibuni ilizindua kampeni ya Global Vax Initiatives yenye lengo la kuhamasisha jamii kupata chanjo ya UVIKO-19 pamoja na kufuatilia wale ambao hawakukamilisha chanjo zenye dozi mbili.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso