NA PASCHAL MALULU-HUHESO BLOG
Dirisha la usajili wa timu zitakazoshiriki
mashindano ya Ndondo Cup ya Clouds FM 2022 limefunguliwa ambalo litadumu kwa
muda wa siku saba (wiki moja) wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Akizungumza na wandishi wa habari za michezo
katika mkutano wa kufungua zoezi hilo mwakilishi na mtangazaji wa kituo cha
Clouds fm Yahya Mohamed (Mkazuzu) amesema Ndondo Cup katika wilaya ya Kahma
itashirikisha jumla ya timu 16.
Ameongeza kuwa michuano ya Ndondo Cup 2022
timu zote zinaruhusiwa kujisajili na idadi ikitimia ya timu 16 zoezi hilo
litafungwa na mchakato wa upangaji wa ratiba na taratibu zingine zitafuata.
Nae mjumbe wa chama cha soka wilaya ya
Kahama (KDFA), Julius Lugobi amewashukuru Clouds Media na Clouds fm kwa kuleta
michuano hiyo katika wilaya ya Kahama kwani itakuwa fursa ya vijana kuonekana
na timu mbalimbali nchini na kupata nafasi kwani Kahama kuna vijana wengi wenye
vipaji lakini walikuwa wanakosa fursa ya kuonekana.
Kwa upande wake katibu mkuu wa chama cha
soka Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) Michael Kaijage amesema walituma maombi kwa
uongozi wa Clouds Media kwa ajili ya kusogeza mkoani Shinyanga michuano hiyo ya
Ndondo Cup na wanashukuru kukubaliwa kwa ombi lao.
Hata hivyo michuano ya Ndondo Cup 2022 ya
Clouds fm bingwa wa mashindano atazawadiwa milioni tano (5,000,000) na mshindi
wa pili milioni tatu (3,000,000) huku yakiongozwa na kauli mbiu ya TWENDE
PAMOJA JIANDAE KUHESABIWA.
No comments:
Post a Comment