KABURI KATIKATI YA BARABARA: FAMILIA YAGOMA KULIHAMISHA, YATAKA MILIONI 30-SIMIYU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 9 June 2022

KABURI KATIKATI YA BARABARA: FAMILIA YAGOMA KULIHAMISHA, YATAKA MILIONI 30-SIMIYU




Familia ya Saguda Madako ya kijiji cha Nkindwabiye Halmashauri ya Wilaya ya Baradi Mkoani Simiyu, imegoma kuhamisha kaburi linalodaiwa kuzikwa mama yao mzazi ambalo lipo katikati ya Barabara katika kijiji hicho kwa madai hadi walipwe kiasi cha Shilingi Milioni 30 na serikali.


Kaburi hilo limejengwa katikati ya Barabara kuu ya Nkololo-Nkindwabiye–Halawa, ambapo familia hiyo imedai mama yao mzazi alizikwa eneo hilo tangu mwaka 1974, na kujengelewa mwaka 2006.


Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa huo David Kafulila wakati akikagua ujenzi wa Barabara hiyo, Meneja Tarura Wilaya, Mathias Mgolozi amemweleza Mkuu huyo wa Mkoa kuwa licha ya kukaa na familia hiyo mara kwa mara kwa ajili ya kuhamisha kaburi hilo lakini imeshindikana.


Mgolozi amesema mara ya kwanza familia hiyo ilitaka Milioni 30 ili kaburi hilo lihamishe, baadaye wakataka Milioni 20, na mara ya mwisho walipunguza na sasa wanahitaji Milioni 1.5.


“Baada ya madai hayo, tulimweleza kwa mujibu wa sheria kuhamisha kaburi familia inapewa kiasi cha Sh. 500,000 na serikali itasaidia kuhamisha kaburi hilo, lakini mpaka sasa familia imegoma,” amesema Mgolozi.


Baada ya hali hiyo Mkuu wa Mkoa, aliagiza kuhamishwa kwa kaburi hilo bila ya kusikiliza uhamuzi wa familia kama inataka au hapana na familia ipewe kiasi hicho cha pesa kama sheria inavyotaka.


“Kama sheria inasema hivyo basi naagiza kaburi hili liondolewa mara moja, endapo ujenzi wa Barabara hii utaaanza kaburi liondolewa familia ikubali isikubali kaburi liondolewe na ujenzi wa barabara ufanyike,” amesema Kafulila.

Chanzo:Globaltvonline

Tazama hapa wafamilia ikizungumza mbele ya mkuu wa Mkoa

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso