Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amefanya ziara katika eneo la Loliondo, Ngorongoro kwa ajili ya kujionea zoezi linaloendelea la uwekaji alama za mipaka, ambapo ameeleza kuridhishwa kwake na kasi iliyopo.
IGP Sirro ambaye alifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella, amefanya ziara hiyo leo Jumatatu Juni 13, 2022 ambapo amesema zoezi la uwekaji alama kwenye pori tengefu lililopo Loliondo wilaya ya Ngorongoro Arusha linakwenda vizuri.
IGP sirro amewataka wanasiasa kuacha kuwaamasisha wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo kuleta uvunjifu wa amani.
"Shida kubwa niwaambie ndugu zangu, Watanzania wenzangu, sisi huwa hatugombani hata siku moja, shida kubwa kuna baadhi ya wanasiasa wanaingilia, wao wana watoto wao wako ulaya wanakula kuku, wanatumia hizi hifadhi zetu kupata faida zao" amesema IGP Sirro
Aidha amewaasa wananchi kuwa watulivu nakushirikiana na serikali katika uamuzi huu wenye lengo la kuhifadhi eneo hilo kwa faida mtambuka za nchi.
"Msikubali kutumika kuchochea vurugu ambazo hazina manufaa kwa pande zote na wala msikubali kutumika kwa niaba ya wale wote wasiotutakia mema kama taifa"amesisitiza IGP sirro
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella alimhakikishia IGP Sirro kuwa Serikali ya Mkoa wa Arusha imejipanga kuhakikisha kuwa zoezi linaendeshwa kwa hali ya utulivu kwa kuzingatia sheria za nchi.
No comments:
Post a Comment