Idadi ya watu waliofariki kwenye ajali ya Costa kugongana na lori lililokuwa limeharibika karibu na eneo la Changarawe, Mafinga mkoani Iringa imefikia 20.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari hiyo iliyokuwa inatoka Dar es Salaam kwenda Mbeya.
Amesema awali, dereva wa costa alipoteza mwelekeo na kuligonga roli ambalo lilikuwa limepata ajali kwenye eneo hilo.
No comments:
Post a Comment