Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kutokana na kutikisika kwa taifa dhidi ya Janga la ugonjwa wa Uviko-19 nchi imepata ahueni huku akitilia wasiwasi kuibuka kwa ugonjwa huo.
Rais Samia ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya mfuko wa fursa kwa wote.
Amesema kwa hivi sasa taifa limepumua ambapo watanzania wameacha kuvaa Barakoa licha ya kuendelea kusikia ugonjwa huo katika mataifa mengine huku akisisitiza kumuomba Mungu janga hilo lisiibuke nchini.
"Barakoa sasa hivi hazivaliwi, nchi imepumua, tunapumua kwa raha hili Dude hatujui litaibuka lini, lakini ujanja ni kuchanja tukachanje ili likikupata lisikusumbue sana na Mungu atuepushie mbali hatujui litaibuka na kasi gani".
Hata hivyo Rais Samia amewataka watu wote ambao bado hawajapata chanjo kuhakikisha wanapata chanjo yake ili kujikinga na janga hilo.
No comments:
Post a Comment