Serikali imewaagiza wakurugenzi wa halmashauri 18 zinazotekeleza Mradi wa Timiza Malengo kusimamia afua mbalimbali za mradi huo, lengo likiwa ni kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa wasichana balehe na wanawake wenye umri wa miaka 10 hadi 24.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene ameyasema hayo kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa vishikwambi kwa walimu wa shule za msingi na sekondari kwenye mradi wa timiza malengo.
Ameyataja mambo wanayotakiwa kusimamia kwa ufanisi ni kuanzishwa na kuimarisha klabu za Ukimwi ambazo zitawezesha wanafunzi kujadili na kujifunza mada zilizowekwa katika vishikwambi na kusimamia matumizi sahihi ya zana kwa uendelevu wa mradi kwenye halmashauri husika.
No comments:
Post a Comment