GHARAMA YA KUJENGA CHOO BORA NI NDOGO KULIKO MATIBABU YA MAGONJWA-AFISA AFYA KAGERA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 23 June 2022

GHARAMA YA KUJENGA CHOO BORA NI NDOGO KULIKO MATIBABU YA MAGONJWA-AFISA AFYA KAGERA




Na Mutayoba Arbogast,Bukoba


Wananchi mkoani Kagera wamehimizwa kuendelea kujenga vyoo bora ili kuepukana na magonjwa kama kuhara, kuharisha na kipindupindu ambayo husababisha gharama maradufu kuyatibu kuliko gharama au nguvu kazi ambazo mtu angetumia kujenga choo bora huku wakati mwingine magonjwa hayo yakisababisha vifo.


Hayo yameelezwa na Afisa afya wa mkoa wa Kagera, Zabron Segeru wakati akiongea na vyombo vya habari wiki hii,ikiwa ni njia mojawapo ya kuhamasishaji ujenzi wa vyoo bora na kuvitumia.


Amesema mkoa wa Kagera umefikia asilimia 99.7 hivi,ikiwa lengo ni kufikia asilimia 100 na kwamba kwa zaidi ya miaka mitatu imekuwepo kampeni kubwa ya kutoa elimu na hata kutumia sheria na sheria ndogondogo,ili kuleta mabadiliko ya kuwa na vyoo bora,na amewahimiza wananchi kushirikiana na wadau wa afya kuhakikisha lengo linafikiwa.


"Kujenga choo bora siyo gharama kubwa.Ni kuchimba shimo,kusakafia,kujenga kuta na paa ambavyo vitamsitiri mtumiaji,na kuweka kifaa cha maji tiririka kunawa mikono,basi", amesema Segeru huku akiongeza kuwa wenye uwezo wanahimizwa vyoo bora vya kisasa.


Amesema baadhi ya watu wanaweza kuwa na choo lakini hawakitumii huku wengine wakiwa na vyoo viwili,kimoja cha hovyo kwa ajili ya watoto au wapita njia huku baba na mama wana choo yao iliyo bora,akisema hii siyo sawa,kwani kika mmoja anatakiwa kutumia choo bora.


Kutozingatia matumizi ya vyoo bora huwaathiri zaidi watoto wadogo chini ya miaka nane,kwa kupata maradhi yatokanayo na uchafu,na hatimaye kudumaa kimwili na kiakili.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso