Mkuu wa wilaya ya Kaliua,Paul Chacha,amemcharukia Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo,kutokana na kitendo cha kuondoa shauri mahakamani la mtoto wa darasa la sita aliyebakwa na mwalimu kisha kupata ujauzito ambao amejifungua huku aliyebaka akibaki huru na kushindwa kuwajibishwa.
Chacha alidai aliyebakwa amejifungua mtoto huku shauri la kesi yake likiwa limeondolewa mahakamani jambo ambalo si haki na ukikuwaji mkubwa wa mamlaka kwa kudiriki kumlinda mharifu pasipo kuhakikisha sheria inashika mkondo wake.
Mkuu huyo wa wilaya anasema,"Hapa Igagala mtoto wa darasa la sita amepewa mimba na mwalimu na imekua bahati mbaya sana na OCD mimi bado napambana na wewe, hilo shauri liliondolewa mahakamani na ninyi mmemrudisha huyo mwalimu mnamlipa mshahara,
mtoto amezaliwa anafanana na mwalimu hana chakukwepa, sasa yule mtoto haki yake nani anailinda!? Anafanyaje?”Alihoji Mkuu wa wilaya.
Akigusia tukio lilivyokuwa Mkuu wa wilaya anasema.“… mwalimu alimwambia nenda kaoshe vyombo nyumbani kwangu utawakuta wenzio baada ya hapo akamnyemelea akamvuta ndani siku hiyo hiyo nakumpa na mimba.
“ OCD tumeshasema huyo mwendesha mashtaka wako hatufai na sio kwa kesi hii ni nyingi tu" alilalama Mkuu wa wilaya ya Kaliua Paul Chacha.
No comments:
Post a Comment