HALMASHAURI ya manispaa ya Bukoba imejizatiti kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinaisha na kuhakikisha watoto wanapata haki zao,ikiwemo fursa ya kupata elimu.
Na Mutayoba Arbogast,Bukoba
Hayo yamesemwa na Afisa maendeleo ya jamii wa Manispaa ya Bukoba,Wanchoke Chinchibera,wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika 16 June,ambayo hufanyika kila mwaka kwa Tanzania kuungana na nchi nyingine za Kiafrika,kukumbuka madhila ikiwemo vifo 2000,majeruhi 1000 na wengine kadhaa ku ulemavu,waliyopata watoto mwaka 1976 huko Soweto,Afrika kusini,wakati watoto walipoandamana kupinga elimu duni na ya kibaguzi waliyokuwa wakipewa na serikali ya kikaburu.
Mwaka 1991 wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa nchi huru za Kiafrika(OAU),walianzisha siku ya Mtoto wa Afrika kukumbuka madhila hayo,na pia kuzuia vitendo vya ukatili kwa watoto.
Maadhimisho hayo yamefanyika uwanja wa Mashujaa(zamani ukiitwa uwanja wa Uhuru)mjini Bukoba,huku kauli mbiu kitaifa ikiwa ni,Tuimarishe ulinzi wa mtoto-Jiandae kuhesabiwa"
Amewakumbusha wasimamizi wa sera na sheria,wazazi ,walezi ,serikali na wadau wengine kuhusu wajibu wao wa kuendelea kulinda,kusimamia na kuimarisha ulinzi na usalama wa mtoto,ambapo amesema kwa upande wa serikali wamekuwa mstari wa mbele,kwa kushirikiana na wadau wengine wa masuala ya watoto,kufuatilia maendeleo yao.
Amesema kwa kipindi cha Januari-Juni 2022 wamefuatilia matukio 92 ya ukatili dhidi ya watoto,ambapo 38 yamefikishwa mahakamani.
Akiainisha vitendo hivyo vya kikatili,Afisa maendekeo huyo ,ameainisha kuwa waliofanyiwa ukatili wa kihisia ni 54,wa kike 43 na wa kiume 11,ukatili wa kiuchumi watoto kufanyishwa kazi 34 kati yao wavulana 30 na wasichana wanne,ukatili wa kingono kwa watoto wa kike watatu,na tukio moja la ukatili wa kimwili kwa mtoto mmoja wa kike.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo,Mstahiki Meya wa manispaa ya Bukoba,amesisitiza kuwa Serikali inajitahidi Sana katika kuhakikisha haki za Watoto zinalindwa ndio maana vipo Vyombo mbalimbali vinavyohusika na Masuala ya Watoto Kama Mahakama ya Watoto, Maafisa ustawi wa Jamii, Madawati ya jinsia polisi, Mabaraza ya Watoto n.k engo kubwa ni Kuhakikisha Watoto wanapata haki zao za msingi.
Wanafunzi John Joseph na Halima Sued wamesema wanaifurahia siku yao kuona serikali inawajali ikiwemo elimu bure,lakini wakapmba pia serikali ingesaidia kugharamia chakula shuleni ili watoto wengi waweze kutimiza ndoto zao,kwani chakula cha mchana mashuleni imekuwa ni tatizo.
Kwa mujibu wa Ripoti ya Wizara ya Mambo ya Ndani Januari-Machi 2021,takwimu za ukatili wa kijinsia nchini,wakiwemo watoto na watu wazima ni kuwa kesi zilizoripotiwa polisi(21,063),watuhumiwa waliohukumiwa(14,278),matukio ya kubaka(19,726),matukio ya kulawiti(3,260).
Matukio mengine ni kuunguzwa moto(198),kutupa watoto wachanga(443),na kipigo ni 4,211
Ni wazi vitendo hivi vya kikatili dhidi ya watoto na watu wazima vinawaathiri watoto kimwili na kisaikolojia na hivyo kuathiri ujifunzaji wa awali na maendeleo yao.
No comments:
Post a Comment