Mshambuliaji wa Klabu ya Geita Gold ya mkoani Geita George Mpole inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara ameibuka mfungaji bora wa ligi kuu (NBC PREMIER) kwa msimu 2021/2022 baada ya kufanikiwa kufunga jumla ya mabao 17.
Na Paschal Malulu - Huheso Digital Blog
Mpole ametwaa ufungaji bora baada ya kumshinda mshambuliaji wa Yanga na raia wa DRC Congo, Fiston Kalala Mayele ambaye ana magoli 16 na idadi hiyo George Mpole ameifikia baada ya kufunga bao moja katika mchezo wa leo wa kuhitimisha msimu 2021/22 dhidi ya Coastal Union katika dimba la Mkwakwani mjini Tanga.
Geita Gold wamelazimisha sare ya bao moja kwa moja ugenini ambapo walikuwa kwanza kupata bao kupitia kwa George Mpole dakika ya 11, na Coastal Union walisawazisha bao hilo dakika 19 lililofungwa na mchezaji wao Rashid Chambo.
MATOKEO YA MICHEZO YOTE LEO YA KUMALIZA MSIMU 2021/22
Azam fc 4-1 Biashara United
Coastal Union 1-1 Geita Gold
Dodoma Jiji 1-0 KMC
Kagera Sugar 0-0 Polisi Tanzania
Mbeya city 1-1 Namungo
Mbeya kwanza 0-0 Simba
Ruvu Shooting 1-0 Tanzania Prisons
Yanga 1-0 Mtibwa Sugar
Hata hivyo baada ya matokeo ya michezo ya leo timu ya Biashara United ya Mara imeshuka daraja kutoka ligi kuu hadi ligi ya Championship msimu ujao 2022/23 ikiungana na timu ya Mbeya kwanza iliyokuwa ya kwanza kushuka daraja baada ya kila timu kucheza michezo 30.
No comments:
Post a Comment