Picha hii haihusiani na tukio hilo.
Mwanaume aliyemuingizia mke panga sehemu za siri kwa tuhuma ya kuchepuka,inadaiwa alimkeketa na sasa anaitwa ngariba wa kiume anayekeketa wanawake.
Mei 25 majira ya saa sita usiku katika Kitongoji cha Nyahende kijiji cha Getarungu kata ya Nyansurura wilayani Serengeti,Gisiri Mrimi (40)inadaiwa alimpiga mke wake jina limehifadhiwa kwa fimbo kisha kumwingizia panga sehemu za siri baada ya kutokea ugomvi baina yao akimtuhumu kwa kutokuwa mwaminifu.
Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Getarungu Jakobo Turuka leo Jumatano Juni 1,2022 amesema,jamii imembatiza Gisiri cheo cha ngariba wa kiume anayekeketa wanawake kwa kuwa ameanza na mke wake.
"Kwa kawaida ngariba wa kiume hutaili wavulana,wakike hukeketa wasichana na wanawake,kwa kitendo chake cha kumwingizia panga mfano wa sime sehemu za mke wake na kumkeketa kimeibua mjadala sana hapa kijijini,"amesema Mwenyekiti.
Amesema,sababu za ugomvi huo zilichangiwa na watu mbalimbali wakiwemo ndugu zake ambao walikuwa wakimpigia simu wakati yuko Katoro Geita kuwa mke wake anachepuka na watu mbalimbali hapo kijijini.
"Kwanza siku hiyo aliambiwa kuwa mkazi mmoja wa kijijini hapo(jina tunalo)anamiliki mke wake,alikimbilia panga ili amuue baada ya kumkosa hasira zikaishia kwa mke na kumpiga kisha akamwingizia panga sehemu za siri na kumkata kama njia ya kumkeketa,niliambiwa nikaenda nikakuta kweli amemkeketa ili apunguze hamu ya kukutana na wanaume,"amesema.
Mmoja wa majirani zake jina tunalo amesema,"watoto walipojaribu kwenda kusuluhisha ugomvi akawatishia amani ikabidi watulie,mke wake baada ya kufanyiwa ukatili huo aliona aibu kusema alipomwingizia panga alimkata kama njia ya kumkeketa,lakini alipoulizwa baadae alikiri kufanyiwa ukatili huo,"amesema.
Amesema,mbali na mgogoro wa kutuhumiwa kuchepuka lakini Gisiri aliporudi alikuta binti yake ametoroshwa kwenda Tarime,hata hivyo baada ya kumrudisha akatoroka kwenda kwa mpenzi wake,akamtuhumu mke kuwa anajua mchakato huo.
"Kwa ujumla yeye ni jirani na ndugu yangu pia,sisi ndugu zake tunataniwa sana kuwa ukoo wetu umevunja rekodi kwa kupata ngariba wa kiume anayekeketa wanawake,"amesema.
Amebainisha kuwa huyo binti yake alifaulu kujiunga Nyansurura Sekondari mwaka 2020 na sasa angekuwa kidato cha pili lakini hakumpeleka shule kwa nia ya kumuoza lakini akatoroshwa na mwanaume bila mahari,kitendo hicho na maelezo ya watu kuhusu mke wake kilimchanganya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Longinus Tibishubwamu licha ya kukiri kuwepo kwa tukio ameomba wananchi kutojichukulia sheria mkononi bali watoe taarifa kwenye vyombo vya dola.
CHANZO:SERENGETI MEDIA CENTER
No comments:
Post a Comment