Msanii wa kizazi kipya Zuhura Othman almaarufu; Zuchu kwa jina la kisanii.Amemsogelea kwa kasi nguli katika Muziki huo,Rajab Abdul Kahali "Harmonize"3 kwa kushika nafasi ya tatu kutazamwa zaidi katika mtandao wa You tube kwa mwezi April Mwaka 2022.
Kinara wa kutazamwa zaidi nafasi hiyo imeendelea kushikiliwa na Nguli katika Muziki wa kizazi kipya nchini Nasibu Abdul "Diamond Platnumz".
Kwa mujibu wa idadi ya watazamaji waliyotembelea akaunti za wasanii wa Tanzania katika Muziki huo,Zuchu amemuwashia taa nyekundu Harmonize aliyeshika nafasi ya pili kwa tofauti ya Watazamaji Milioni 4.9.
Zuchu anayetamba na nyimbo;Sukari,Nisamehee na Kwalu hana miaka mingi katika tasnia ya Muziki huo,lakini amepata umaarufu mkubwa na kujikuta akipata wafuasi wengi hadi katika mitandao ya Kijamii,ambapo katika mtandao wa you tube kwa mwezi April ameshika nafasi ya tatu.
Kwa kushika nafasi hiyo imemuwezesha kwa mara ya kwanza kumpiku Msanii aliyenaye label moja ya Wasafi,aitwae Raymond Shaban Mwakyusa "Rayvanny"huku akimuacha kwa nafasi tano,Nguli zaidi katika Muziki huo Ali Kiba.
𝐑𝐚𝐲𝐯𝐚𝐧𝐧𝐲 ambaye katika orodha ya wanamuziki waliotazamwa zaidi katika mtandao wa youtube kwa mwezi April Mwaka huu,ameanguka kwa nafasi mbili kwa kushika nafasi ya tano kutoka ya tatu mwezi uliiopita
Orodha ya wanamuziki kumi wa Tanzania waliopata idadi kubwa ya watazamaji katika mtandao wa youtube kwa mwezi April 2022,ipo kama ifuatavyo;
1. Diamond Platnumz 40.3M
2. Harmonize 13.8M
3. Zuchu 8.9M
4. Marioo 8.1M
5. Rayvanny 7.3M
6. Mbosso 7.2M
7. Zabron Singers 4.2M
8. Alikiba 3.5M
9. Martha Mwaipaja 3M
10. Nandy 2.9M
No comments:
Post a Comment