WAZIRI MKUU MSTAAFU FREDRICK SUMAYE AOMBA KUWA MJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI CRDB - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday, 22 May 2022

WAZIRI MKUU MSTAAFU FREDRICK SUMAYE AOMBA KUWA MJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI CRDB



Waziri Mkuu katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tatu, Fredrick Sumaye, ameomba kuchaguliwa kwa mara nyingine kuwa mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, licha ya kuwahi kujiuzulu katika wadhifa huo kwa maslahi ya benki hiyo.


Akiomba kura,Waziri Mkuu huyo mstaafu,alidai kwamba alipata kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya CRDB,lakini aliwajibika kuondoka katika wadhifa huo kutokana na kuibuka vitisho ambavyo havikuwa na afya  na ambavyo pindi angeendelea kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa CRDB,ingeathiri maendeleo ya benki hiyo.


Alisema ameshawishika kujitokeza kuomba nafasi hiyo baada ya kujiridhisha kutokuwepo kwa tishio dhjidi yake kutokana na hali ya mambo kwa kipindi hiki kutokuwa na dalili za kudhoofisha taasisi pindi akiwa mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.


Hata hivyo hakutoa ufafanuzi wa kina juu ya vitisho hivyo,licha ya wana hisa kuhitaji kutambua kwa kina juu ya vitisho anavyodai zaidi ya kudai kipindi hiki hali ni shwari hivyo hana budi kujitokeza na kuomba wadhifa huo kwa mara nyingine.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso