Makumi ya watu wameuawa baada ya watu wenye silaha kuvamia mgodi wa dhahabu huko Djugu katika jimbo la Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo siku ya Jumapili.
Shirika la habari la AFP limemnukuu afisa mmoja wa eneo hilo akisema kuwa miili 29 ilikuwa imetolewa kutoka kwenye mgodi huo na Miongoni mwa waliofariki ni mtoto wa miezi minne.
Katika taarifa, wizara ya mawasiliano imelilaumu kundi la waasi la Codeco kwa shambulio hilo na Serikali inabainisha kwamba kitendo hicho ni cha kumi na moja cha kinyama na cha woga cha magaidi wa Codeco dhidi ya watu wasio na hatia.
Kundi la Codeco hapo awali limeshutumiwa kufanya uvamizi dhidi ya raia katika miezi ya hivi karibuni na linalaumiwa kwa kuua takriban watu kumi na wawili kwenye kanisa mnamo Machi, na wengine 60 mnamo Februari.
CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment