WATOTO 450,000 KUPEWA MATONE YA CHANJO YA POLIO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 18 May 2022

WATOTO 450,000 KUPEWA MATONE YA CHANJO YA POLIO



Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akimpa mtoto matone ya Chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kupooza (Polio) wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga.


Mjema amesema takribani watoto 450,000 wenye umri chini ya miaka mitano mkoani Shinyanga wanatarajiwa kufikiwa/kupatiwa chanjo ya Polio kuanzia Mei 18 hadi Mei 21,2022. Chanjo hiyo itatolewa nyumba kwa nyumba na kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya watoto likiendeshwa na timu ya wataalamu 855.


“Niwatoe hofu wazazi wa Mkoa huu wa Shinyanga, Chanjo hii ya Polio ni salama kabisa na haina madhara yoyote, hakikisheni watoto wanapewa chanjo hii, zoezi litafanyika nyumba kwa nyumba na kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya watoto”,amesema.


Polio ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi cha Polio ambacho huenezwa kwa kula chakula na kunywa maji yaliyochafuliwa na kinyesi cha mtu mwenye ugonjwa huo.


Ugonjwa wa Polio huathiri zaidi watoto wenye umri chini ya miaka mitano ambapo dalili za ugonjwa huu ni Homa, mafua,maumivu ya mwili,kichwa na shingo au ulemavu wa ghafla wa viungo vya mwili.


Ugonjwa wa Polio hushambulia mishipa ya fahamu hatimaye husababisha kupooza kwa misuli hasa ya miguu, mikono au yote kwa pamoja na mwingine misuli ya kifua inayosaidia kupumua na kusababisha kifo. Polio husababisha ulemavu wa kudumu.


"Kumbuka kila tone la chanjo ya Polio litaiweka Tanzania salama dhidi ya ugonjwa wa kupooza...Mpe Mtoto Matone...Okoa Maisha"

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso