Na, Sada Salum
Wananchi wa Kata ya
Nyasubi katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wamelitaka jeshi la polisi
kuonesha ushirikiano kwa wananchi pindi matukio ya kihalifu yanapojitokeza.
Wamesema hayo April 29, 2022 wakati wa
mkutano wa hadhara uliowahusisha wananchi wa Kata hiyo, viongozi wa Kata pamoja
na jeshi la polisi Wilaya ya Kahama ambapo wamedai kuwa jeshi la polisi
limekuwa likichelewa kufika eneo la tukio na kupelekea wahalifu kutokukamatwa.
Hamad Mnubwa mkazi wa
Mtaa wa Nyakato, amesema polisi hawana ushirikiano na raia pindi inapotokea
taarifa za uhalifu hivyo wanaliomba jeshi hilo kuwa na ushirikiano na wananchi.
Nae Juma Ngoma mkazi wa
Mtaa wa Nyakato mwisho amesema baadhi ya maafisa polisi wamekuwa hawana majibu
mazuri kwa wananchi ambao wanatoa taarifa za uhalifu.
Kwa upande wake
mwakilishi wa Jeshi la Polisi Kahama ambaye ni mkuu wa Upelelezi Manispaa ya
Kahama ASP Maro amesema wananchi wanapaswa kuwa na ulinzi shiriki wakati huu
ambao kituo cha polisi kikiwa hatua ya ukamilishaji kwenye Kata hiyo.
Hata hivyo Afisa polisi jamii Mkaguzi amewataka
vijana kujitokeza katika kufaya ulinzi shirikishi huku akiwataka wananchi kutii
sheria kwa kutojichukulia sheria mkononi pindi wanapowakamata wezi au wahalifu.
MWISHO
No comments:
Post a Comment