WANANCHI WALALA NJE KISA MATETEMEKO, WAZIRI BITEKO AUNDA TUME KUCHUNGUZA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday, 1 May 2022

WANANCHI WALALA NJE KISA MATETEMEKO, WAZIRI BITEKO AUNDA TUME KUCHUNGUZA









Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko ametoa maagizo kwa wataalam kutoka Taasisi ya jiolojia na utafiti wa madini Tanzania kuweka kambi ya kufanya uchunguzi dhidi ya tetemeko la ardhi katika kijiji cha Ulowa Namba 8 halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.


Biteko amebainish hayo Jana April 30, 2022 mara baada ya kutembelea katika eneo hilo kutokana na wananchi kujawa na hofu baada ya nyumba zao kuanza kupasuka nyufa kutokana na mitetemo inayotokea.


Baadhi ya wananchi wanahofia kuwa hali hiyo inasababishwa na wachimbaji wa madini katika migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu kuwa wakati wa ulipuaji wa miamba inapelekea hali hiyo.


Waziri Biteko amesema hofu iliyopo kwa wananchi kuwa migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi ndio inasababisha hali hiyo sio kweli kutokana na umbali uliopo ambapo umbali uliopo ni Zaidi ya kilomita 80 hadi 100 kufika kwenye migodi hiyo.


Amesema uchunguzi wa mitetemo inayotokea mara kwa mara katika eneo hilo itachunguzwa kwa siku 14 ili kubaini huku akisema kama taarifa zinavyoelezwa kuwa ni matetemeko sio kweli kutokana nan chi kuwa na vifaa vya kubaini hivyo kwa sasa haijabainiwa kwenye mitambo hiyo.


Aidha, Waziri Biteko amewataka wananchi kuwa watulivu kutokana na hali hiyo ambayo imejaa taharuki eneo hilo na kubainisha kuwa kuna aina mbalimbali ya matetemeko yanayoweza kusababishwa na hali hiyo.


MWISHO



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso