Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema mkoani Mwanza, Binuru Shekidele amesema ameanza kufuatia ili kubaini sababu za wananchi kufunga ofisi ya mtendaji na menyekiti wa Kijiji cha Bitoto wilayani humo.
Juzi Jumatatu Mei 2 mwaka huu baadhi ya wananchi walifunga ofisi hiyo wakidai hawana imani na viongozi hao kutokana na matumizi ya Sh3 milioni walizochanga kwa ajili ya ujenzi wa lambo la maji katika kijiji hicho.
Leo, akizungumza Shekidele amesema kwa sasa mamlaka zinaendeleaa na uchuguzi ili kubaini ukweli wa taarifa hizo na baadaye watakuja kwa wananchi kitoa taarifa.
Ametoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi endapo kukikokea sintofahamu yoyote juu ya mtumishi wa umma wafike ofisini kwake kutoa malalamiko yao na watayafanyia kazi.
Mkazi wa Kijiji cha Bitoto, Philipo Mtobela amesema waliamua kufunga ofisi hiyo kutokana na viongozi hao kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha zilizochangwa na wananchi.
Kutokana na tuhuma hizo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Bitoto Busweru Sangija alikanusha tuhuma hizo huku akidai kuwa wananchi hao hawahudhurii kwenye mikutano ya hadhara ambayo inatumika kutoa taarifa za matumizi ya fedha hizo.
Chanzo:mwananchi
No comments:
Post a Comment