Rais Samia amtoa agizo hilo wakati akifungua barabara ya Nyahua-Chanya yenye km 85.4 katika kijiji cha Tura, Wilaya ya Koga Mkoani Tabora leo tarehe 18 Mei, 2022 ambapo amesema anasikitishwa na baadhi ya wananchi kuhujumu miundombinu hiyo.
"nasikitishwa sana na uhalibifu huu wa miundombinu, mtu anaiba Sola na Taa huo ni uhujumu uchumi na jeshi la polisi liwasake na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ili wachukuliwa hatua, hizi taa mnaweza kuzitumia kwa ajili ya maendeleo miundombinu hii ni yenu wenyewe".
"Tunakopa mikopo ya masharti nafuu kwa ajili ya maendeleo yenu wenyewe itunzeni hii miundombinu na waofanya haya mnaomajumbani kwenu wasemeni".
Hata hivyo katika hotuba yake Rais Samia amesema watu wasiofahamika wameweza kung'oa nguzo za panel za sola sambamba na kuiba Taa hivyo watu hao wasakwe huku wakiwaomba wananchi kutoa ushirikiano.
No comments:
Post a Comment