WALIOHAMA KWA BARUA ZA KUGUSHI KURUDISHWA WALIKOTOKA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 16 May 2022

WALIOHAMA KWA BARUA ZA KUGUSHI KURUDISHWA WALIKOTOKA



WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Innocent Bashungwa amemuagiza Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia TAMISEMI, Ramadhani Kailima kuwafuatilia watumishi 12 mkoani Tanga waliogushi barua za uhamisho na mara moja warudishwe kwenye vituo vyao vya kazi.


Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo leo Jumatatu Mei 16, 2022 wakati wa Kikao na Waandishi wa habari kuhusu Matokeo ya Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2020/21.


Amesema kuwa watumishi hao 12 wachukuliwe hatua stahiki za kinidhamu kwa suala la kugushi nyaraka za Serikali.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso