Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa ameagiza kazi ya kukusanya ushuru wa maegesho ya magari (Parking) iliyokua chini ya Wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) kurudishwa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Waziri Bashungwa ametoa maagizo hayo leo wakati wa Kikao chake na Uongozi wa TARURA na Mawakala wa Ukusanyajinwa ushuru wa maegesho kwenye Halmashauri mbalimbali nchini.
Aidha Mje. Bashungwa amemuelekeza Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe kusimamia makabidhiano ya chanzo hicho haraka baina ya TARURA na Mamlaka za Serikali za Mitaa
Amesema naona malalamiko toka kwa Wananchi hayaishi kuhusiana na chanzo hiki na Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan hafurahishwi na malalamiko haya ya wananchi kila mara na pia hili la ukusanyaji wa Parking sio jukumu la msingi la TARURA hivyo nalirudisha halmashauri ili ninyi TARURA mkasimia kutengeneza barabara na miundombinu kama hiyo.
Ameongeza kuwa nitapenda kuona sasa TARURA mkielekeza nguvu kwenye kuimairisha miundombinu ya barabara za mijini na vijijini na mkafungue barabara na kufika kusikofikika, madaraja yakajengwe, makalavati ili kurahisha usafiri kwa wanannchi wetu.
‘TARURA kwa mwaka wa fedha unaokuja nimewaombea Bajeti ya kutosha na nimewaelekeza mtangaze Zabuni mapeema ili mwaka wa fedha unapoanza uende sambamba na ujenzi wa miundombinu hiyo.
Na Katika hili la usimamizi wa miundombinu ntawapima Mameneja wa Mikoa kila baada ya miezi mitatu kwa kigezo cha ufanisi katika kuboresha miundombinu ya eneo husika, alisisitiza Bashungwa
No comments:
Post a Comment