Serikali imetangaza kiwango kipya cha kikotoo cha mafao ya mkupuo ambapo sasa ni asilimia 33 kwa mifuko yote ya hifadhi ya jamii.
Kauli hiyo imetolewa leo Alhamis Mei 26, 2022 na Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Profesa Jamal Katundu.
Amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya makubaliano kati ya Serikali, Chama cha Waajiri Nchini (ATE) na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) bada ya kusitishwa kwa kanuni zilizotengenezwa Desemba 28 mwaka 2018.
Profesa Katundu amesema wamekubaliana kikokotoo limbikizi kitakuwa 1/580 kama ilivyokuwa kwa mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na ilikuwa mifuko ya PPF, GEPF na baadhi ya wanachama wa iliyokuwa PSPF na LAPF.
"Makadirio ya mika 12.5 ya kuishi baada ya kustaafu kama ilivyokuwa kwa mfuko wa NSSF na ilivyokuwa kwa mfuko wa NSSF na iliyokuwa PSPF na LAPF," amesema.
Amesema mshahara wa kukotolea mafao ya pensheni utakuwa wastani wa mishahara bora ya miaka mitatu ndani ya miaka 10 kabla ya kustaafu.
Profesa Katundu amesema umri wa kustaafu kwa lazima utaendelea kuwa miaka 60.
Amesema kikotoo hicho kitaanza kutumika Julai Mosi mwaka huu.
CHANZO:MWANANCHI
No comments:
Post a Comment