Zaidi ya visa 80 vya ugonjwa wa Monkeypox vyathibitishwa katika angalau nchi 12.
Shirika la Afya Ulimwenguni limesema visa vingine 50 vinavyohofiwa kuwa ni monkeypox vinachunguzwa - bila kutaja nchi yoyote - na kuonya kuwa visa zaidi vinaweza kuripotiwa.
Mpaka sasa maambukizi ya ugonjwa huio unaoharibu gonzi yamethibitishwa katika nchi tisa za Ulaya, pamoja na Amerika, Kanada na Australia.
Monkeypox hupatikana sana katika sehemu za mbali za Afrika ya Kati na Magharibi.
Ni maambukizo ya nadra ya virusi ambayo kwa kawaida huwa hafifu na ambayo watu wengi hupona baada ya wiki chache, kwa mujibu wa wataalam.
Virusi hivyo havisambai kwa urahisi kati ya mtu na mtu na hatari ya kuambukiza wagtu wengi zaidi inatajwa kuwa ni ndogo sana.
Hakuna chanjo mahususi ya Monkeypox, lakini chanjo ya ndui hutoa kinga ya 85% kwa kuwa virusi hivi viwili vinafanana kabisa.
CHANZO MUUNGWANA BLOG
No comments:
Post a Comment