Soko la Vetenari lililopo Temeke, Dar es Salaam limeungua kwa moto usiku wa kuamkia leo Mei 30, 2022 huku vibanda 250 kati ya 453 vimeteketea, ikielezwa kuwa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.
Akidhibitisha kutokea kwa moto huo, Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Zimamoto Temeke, Mrakibu Msaidizi Michael Bachubira amesema jitihada za kuuzima moto huo na kudhibiti usisambae maeneo mengine zimefanyika.
Akizungumza baada ya kutembelela soko hilo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema serikali itachukua hatua za haraka kuhakikisha wafanyabiashara katika soko hilo wanarejea sokoni hapo na kuendelea na shughuli zao.
RC Makalla amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo kuchukua hatua za haraka kushugulikia suala hilo.
Soko hilo la Vetenari limeungua moto likiwa na jumla ya wafanyabiashara 803.
Hii ni mara ya nne kwa masoko Jijini Dar es Salaam kuungua kwa mwaka huu ambapo mwezi Februari soko la Mbagala liliungua, na Soko la Karume liliungua mara mbili mwezi Januari na Aprili.
No comments:
Post a Comment