Zoezi la utoaji chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri wa miaka 0-5 wilayani Kahama mkoani Shinyanga lililotarajia kufanyika tarehe 28 April hadi Mei 01 mwaka huu limesogezwa mbele hadi Mei 12, 2022.
Akizungumza Ofisini kwake na Huheso fm leo Mei 05 Katibu tawala Wilaya ya Kahama, Timoth Ndanya amesema zoezi la chanjo ni nyeti kwa watoto hao na sababu ya kusogezwa mbele ni kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao hivyo chanjo hiyo itafanyika.
Amesema wananchi wanalojukumu la kuendelea kujiandaa na zoezi hilo na kuwataka wazazi na walezi kushiriki kikamilifu zoezi hilo ambalo lina manufaa makubwa kwa watoto kwani lina lengo la kuwakinga dhidi ya ugonjwa huo wa Polio.
Hata hivyo zoezi hilo litazinduliwa kimkoa katika Wilaya ya Kahama ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Sophia Mjema.
No comments:
Post a Comment