Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Sheikh Khalifa bin Zayed Al-Nahyan, amefariki dunia akiwa na miaka 73, baada ya kuugua kwa miaka kadhaa.
Kuna uwezekano nafasi ya Sheikh Khalifa ambaye hakuwa akionekana sana hadharani, ikachukuliwa na kaka yake mrithi wa kiti cha ufalme wa Abu Dhabi, Mohammed bin Zayed, ambaye tayari alikuwa akionekana kama mtawala mkuu wa Falme hizo za Kiarabu.
Wizara inayohusika na masuala ya rais imetangaza siku 40 za maombolezo, huku bendera zikipepea nusu mlingoti kuanzia leo na kusitishwa kwa kazi katika sekta ya umma na binafsi kwa siku tatu za mwanzo.
Sheikh Khalifa alichukua madaraka Novemba mwaka 2004, akimrithi baba yake kama mtawala wa 16 wa Abu Dhabi, ambayo ni tajiri zaidi kati ya Falme saba za shirikisho hilo.
Rais wa Marekani, Joe Biden ametuma salamu za rambirambi kwa Umoja wa Falme za Kiarabu kufuatia kifo hicho.
chanzo:DW
No comments:
Post a Comment