NECTA YATOA ONYO MTIHANI WA KIDATO CHA SITA UNAOANZA KESHO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday, 8 May 2022

NECTA YATOA ONYO MTIHANI WA KIDATO CHA SITA UNAOANZA KESHO



Jumla ya watahiniwa 95,955 kutoka shule za sekondari 841 na vituo vya kujitegemea 250 wanatarajia kuanza mitihani yao ya kumaliza kidato ya sita kesho Jumatatu Mei 9, 2022 na kumaliza Mei 27.

Pia watahiniwa 9,670 kutoka vyuo 70 wamesajiliwa kufanya mitihani ya mwisho ya kozi ya ualimu katika ngazi ya stashahada na cheti.

Hayo yameelezwa leo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Dk Msonde amesema kati ya watahiniwa wa kidato cha sita 85,531 ni wale wa shule na 10,424 ni wa kujitegemea.

"Kati ya hao wanaume ni 47,859 ni wavulana sawa na asilimia 55.96 na wasichana ni 37,672 sawa na asilimia 44.04," amesema Dk Msonde.

"Pia watahiniwa wenye mahitaji maalumu wapo 151 na kati yao 136 ni wenye uoni hafifu na 15 ni wasioona."


Kati ya watahiniwa wa kujitegemea 10,424 waliojisajili, wanaume ni 6,546 sawa na asilimia 62.80 na wanawake ni 3,878 sawa ana silimia 37.20 na asiyeona ni mmoja.

Kati ya walimu wataketi kufanya mtihani huo, 4,560 ni ngazi ta stashahada na 5,110 ni ngazi cheti.

Dk Msonde ameaema baraza halitasita kukifuta kituo chochote cha mitihani endapo litajiridhisha kuwa uwepo wake unahatarisha usalama wa mitihani ya Taifa.

"Baraza linatumia nafasi hii kuwataka wamiliki wa shule wote kutambua kuwa shule ni vituo maalumu vya mitihani na hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani katika kipindi chote cha ufanyaji mitihani hii," amesema Dk Msonde.

CHANZO:MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso