The Cashewnut Board of Tanzania (CBT) Temporary vacancies, May 2022 is a corporate body established by the Act No. 18 of 2009.
It is entrusted with the responsibility of regulating the development of the Cashew Industry in Tanzania in undertaking its mandated roles.
The Cashewnut Board puts more emphasis in improving efficiency and effectiveness in the cashewnut sub-sector in order to meet requirements of different stakeholders thereby enabling them to contribute to the national development.
The Tanzania Cashew Board consists of the Board of Directors, the Director General, the Legal Unit, the Internal Audit Unit, the Procurement Unit and supply, Directorate of Finance and Administration, Directorate of Agriculture and Discrimination, Marketing Directorate and Regulation quality plus five (5) branches located in Dar es Salaam, Tanga, Tunduru, Lindi and Manyoni as well one (1) station in Morogoro.
The Vision is To be a competent institution for providing policy, regulatory and technical advice for a modern efficient and economically viable and sustainable Cashewnut industry by year 2025.
TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MUDA
Bodi ya Korosho Tanzania ni Taasisi ya umma iliyoko chini ya Wizara ya Kilimo iliyoanzishwa kwa Sheria ya Tasnia ya Korosho Na. 18 ya Mwaka 2009. Bodi hii imekasimiwa jukumu la kusimamia maendeleo ya zao la korosho katika ngazi zote za uzalishaji, ubanguaji/usindikaji, masoko na utafiti ili kuhakikisha kuwa zao la korosho linatoa mchango wake katika kuinua pato la mkulima wa zao hili na Taifa kwa ujumla.
1. WASIMAMIZI WA MASHAMBA YA KOROSHO - MANYONI
A. SIFA ZA WAOMBAJI
- Awe Mtanzania na umri kuanzia Miaka 18 - 40;
- Awe amehitimu kidato cha IV na kufaulu masomo ya Kiswahili na Kiingereza;
- Awe na Cheti cha Stashahada ya Kilimo au sifa zinazofanana na hizo kutoka Chuo kinachotambulika na serikali
- Awe mwadilifu, mtiifu na mwenye akili timamu;
- Awe Mkazi wa Mkoa wa Singida na maeneo mengine ya jirani
B. MAJUKUMU YA KAZI YA WASIMAMIZI WA MASHAMBA YA
KOROSHO
- Kushirikiana na wakulima kuendesha mashamba darasa na mashamba ya majaribio.
- Kutembelea wakulima na vikundi vya wakulima katika mashamba yao ya korosho na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya mbinu bora za kisasa za kilimo biashara.
- Kuwafundisha na kuwaeleza wakulima juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu , mbolea , madawa na zana za kilimo.
- Kukusanya na kutunza takwimu za hali ya kilimo cha Korosho.
- Kutoa taarifa juu ya dalili za kuwepo visumbufu wa Korosho.
- Kuandaa na kutumia daftari la kilimo katika kutekeleza majukumu ya kila siku.
- Kuandaa taarifa ya utekelezaji ya kila mwezi na kuiwasilisha Tawi la Manyoni.
Mshahara
Mshahara wa kazi hii kwa mwezi ni Tsh 450,000/=
Ajira hii ni ya mkataba wa miezi Sita sio ya kudumu.
Maombi yote yatumwe kwa anuani hii kabla ya tarehe 11.05.2022 saa 10:00
jioni.
MKURUGENZI MKUU,
BODI YA KOROSHO TANZANIA,
S.L.P 533,
MTWARA
info@cashew.go.tz
No comments:
Post a Comment