Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limewataka wazazi na walezi kuhakikisha kuwa watoto wao wanaomba nafasi za astashahada na Stashahada kwenye vyuo vilivyoorodheshwa kwenye kitabu cha mwongozo wa udahili kwa mwaka wa masomo 2022/2023.
Rai hiyo imetolewa hii Leo na Mkurugenzi Udhibiti, Ufatiliaji na Tathimini Jofrey Okele Mara baada ya baraza kutangaza kuanza Kwa udahili wa wanafunzi Kwa ngazi ya astashahada na Stashahada Kwa kozi zote zinazotolewa na vyuo mbalimbali.
"Kwa sasa usajili unatajwa kuhusisha wahitimu wote wa Elimu ya sekondari na vyuo vyenye sifa za kujiunga na kozi zilizotajwa wakiaswa kufanya maombi Kwa umakini Ili kupata nafasi Kwa kutimiza vigezo na sifa zilizotangazwa." amesema Jofreu Okele - Mkurugenzi Udhibiti Ufuatiliaji na Tathimini - NACTVET.
Aidha baraza limesisitiza kuwa wanafunzi waliopangiwa nafasi za masomo na Ofisi ya Rais -TAMISEMI wafanye moja kwa moja mawasiliano vyuoni huku masomo yakitarajiwa kuanza Oct 18,2022.
Udahili kwa wanafunzi kwa ngazi tajwa umefunguliwa rasmi hii leo Mei 24,2022 hadi tarehe 30 Julai, 2023 huku wanafunzi wa program za Afya na Sayansi Shirikishi wakitakiwa kuwasilisha maombi ya pamoja.
CHANZO:EATV
No comments:
Post a Comment