Mwandishi habari wa shirika la utangazaji la Aljazeera ameuwawa leo wakati akiripoti katikati ya makabiliano baina ya wanajeshi wa Israel na Wapalestina kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi.
Wizara ya afya ya Palestina imesema mwandishi huyo habari wa idhaa ya kiarabu ya Aljazeera Shireen Abu Aqleh mwenye umri wa miaka 51, alipata majereha ya risasi ya kichwa na alifariki dunia muda mfupi baada ya kushambuliwa.
Taarifa iliyotolewa na Al-Jazeera imesema vikosi vya Israeli ndiyo vimempiga risasi na kumuua mwandishi huyo.
Al-Jazeera imetoa mwito kwa Jumuiya ya Kimataifa kulaani na kuviwajibisha vikosi vya Israel kwa kumlenga na kumuua kwa kudhamiria mwandishi huyo wa habari.
Kwa upande wake jeshi la Israel limesema linashuku kwamba Abu Aqleh alipigwa risasi na wanamgambo wa upande wa Palestina na limearifu kuwa uchunguzi umeanzishwa kubaini ukweli.
CHANZO:DW
No comments:
Post a Comment