MSHAHARA ZANZIBAR WAONGEZWA KWA 15.6% - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 9 May 2022

MSHAHARA ZANZIBAR WAONGEZWA KWA 15.6%

 

RAIS DKT MWINYI WA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyin ametangaza ongezeko la Mshahara kwa 15.6% ambapo ongezeko hilo litazingatia mfumo wa uzoefu, elimu na uzoefu wao katika kazi. Serikali imetenga Tshs Bilioni 12.7 kwa mwezi sawa na Tshs Bilioni 153 kwa mwaka ili kugharimia utekelezaji huo.


Kutokana na utaratibu huu mtumishi aliyeajiliwa kima cha chini cha mshahara Tshs kutoka 300,000 mpaka Tshs 347,000 kwa mtumishi mpya aliyeajiliwa mwaka 2019 ikiwa ni ongezeko la 15.6%, Mtumishi wa ngazi ya cheti katika masomo ya Art aliyeajiliwa mwaka 2019 Mshahara wake utapanda kutoka Tshs 321,000 hadi kufikia Tshs 382,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 19  


"Ongezeko hilo litasaidia kujikimu kimaisha uwezo wa mfanyakazi na kuondoa kilio cha muda mrefu kwa watumishi wa umma ambapo elimu na uzoefu wao wa kazi haukuwa ukijitokeza waziwazi katika marekebisho ya mshahara kwa vipindi vilivyopita" Amesema Dkt Mwinyi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso