MOROCCO YAONGEZA MSHAHARA KWA 16%, KENYA 12% - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday, 1 May 2022

MOROCCO YAONGEZA MSHAHARA KWA 16%, KENYA 12%





Serikali ya Morocco imetangaza mipango ya kuongeza kima cha chini cha mishahara ya watumishi wa umma kwa 16% na kile cha wafanyakazi wengine kwa 10%.


Ongezeko la 10% litapunguzwa kwa muda wa miaka miwili, ikishuhudia ongezeko la 5% mnamo Septemba 2022 na lingine 5% kuruka mwaka mmoja baadaye, kwa mujibu wa Morocco World News.


Ongezeko hilo lililopendekezwa lilikuwa sehemu ya makubaliano kati ya serikali, vyama vya wafanyakazi na shirikisho la waajiri, kulingana na shirika la habari la Reuters.


Wananchi pia wataona ongezeko la posho za familia kwa wale wenye watoto zaidi ya watatu


Wakati huo huo Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameongeza kima cha chini cha mshahara wa wafanyakazi kwa asilimia 12, kuanzia Mei 2022.


Rais Uhuru alitoa tangazo hilo Jumapili, Mei, alipoongoza Wakenya kusherehekea Siku ya Wafanyakazi mwaka huu katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, ambapo maafisa wa muungano walimtaka azingatie maslahi ya wafanyakazi.


Rais Kenyatta alisema uamuzi huo unalenga kuongeza nguvu kazi ya nchi dhidi ya kupanda kwa gharama ya maisha kunakosababishwa na sababu kadhaa za kiuchumi za nje.

Chanzo:BBCSWAHILI

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso