MGEJA ATOA USHAURI KWA SERIKALI KUTOKOMEZA PANYA ROAD CHOKORAA. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 11 May 2022

MGEJA ATOA USHAURI KWA SERIKALI KUTOKOMEZA PANYA ROAD CHOKORAA.

 

MWENYEKITI wa Tanzania Mzalendo Foundation,Khamis Mgeja,amezishauri wizara tatu katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano kukutana na kufanya kikao cha kuhakikisha wanatokomeza watoto wa mitaani almaarufu kwa jina la chokoraa,ambao amedai ndio chimbuko la kikundi cha vijana waharifu.

 

Kikundi cha Vijana  hao waharifu  ambao wamekuwa tishio na kuzua taharuki kubwa kwa wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam,kutokana na matukio ya kiharifu wanayoyafanya ya kupoka mali za watu na kujeruhi,wanaotambulika jijini kwa jina la Panya Road ana imani maeneo mengine nchini wanaitwa vibaka.

 

Hivyo kutokana na kuamini chimbuko la Panya Road linatokana na watoto wa mitaani ni vyema,kupitia wizara ambazo zinaguswa kwa namna moja ama nyingine na Chokoraa,kuketi na kutafuta njia sahihi ya kuwaondoa ikiwemo kuwarejesha majumani kwao kwa wazazi na walezi wao.

 

 Akiongea na vyombo vya habari,Mgeja aliungana na Watanzania wengine kulaani matukio yanayotendwa na Panya Road,ya kuvamia baadhi ya jamii ya Jijini la Dar E S Salaam kisha kuwaibia huku wakiwaacha wamewajeruhi na baadhi yao kupata ulemavu wa maisha.

 

Mgeja aliwataja Mawaziri wanaostahiki kuketai pamoja na kupata ufumbuzi wa kuwatokomeza Panya Road sambamba na kuwaengua wataoto wa mitaani,kuwa ni Waziri wa Tamisemi,Waziri wa Mambo ya Ndani na Waziri wa Maendeleo ya Jamii.

 

Alisema chokoraa wamekithiri mitaani kila mikoa hapa nchini,ambao matendo yao yamekuwa yakikiuka maadili ya jamii,ikiwemo kufanya uharifu mdogomdogo ambapo kila umri unavyokuwa ndivyo wanavyokomaa,na si ajabu Panya Road kuzagaa nchi nzima.

 

Hivyo aliomba Serikali kuwa na mpango mkakati kupitia wizara hizo kuhakikisha wanakabiliana na Panya Road ama kama wanavyoitwa jina la Vibaka katika maeneo mengine nchini,ambao wameitia khofu jamii katika maeneo mbalimbali nchini.

 

Aidha aliomba Serikali kuwasiliana na viongozi wa kiimani,kuhubiri suala la upendo na maadili katika nyumba zao za ibada kwa kutoa kipaumbele suala la malezi ili kutokomeza watoto wa mitaani,sambamba na kuweka umuhimu wa ulinzi shirikishi ili kukabiliana na vitendo vya kiharifu.

 

Aliendelea kutoa ushauri kwa viongozi kuanzia ngazi mitaa,vijiji,Kata,wilaya hadi Taifa,kutongoja kila jambo litolewe muongozo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan,mathalani la Panya Road,kwani anamajukumu mengi ya Taifa.

 

Mgeja aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga,alisisitiza suala la wizara hizo kuketi ili kuwa na mkakakti wa Kitaifa wa kutokomeza watoto wa mitaani ambao alidai ni bomu ambalo lisipodhibitiwa kipindi hiki litakuwa na athari kubwa kipindi kijacho.

 

“Inasikitika viongozi wanasubiri matukio yatokee,ndipo wajitokeze kusema badala ya kuyadhibiti yasitokee,huu ni udhaifu mkubwa wa kioungozi,”alisema Mgeja.

 

Aidha Mgeja alisema kupitia ofisi ya Waziri Mkuu,ni vyema Halmashauri za Wilaya,Miji,Manispaa na Majiji kutenga bajeti za ulinzi na usalama kwa kushirikiana na serikali kuu sambamba na kutenga maeneo maalumu ya vituo vya kuwafunza ujuzi,kazi na maadili vijana wa mitaani.

 

Alisisitiza ni  budi kuwepo mpango mkakati na endelevu juu ya kuwanusuru chokoraa ikiwemo kuwarejesha kwa wazazi wao,vinginevyo Serikali kupitia Hamashauri za wilaya,Miji,Manispaa na Majiji kutenga maeneo maalumu ya kutoa elimu ya ujuzi ili kukabiliana na changamoto za maisha.

 

Alidai kushangazwa na baadhi ya watendaji wa serikali kushindwa kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan,kukabiliana na matukio ya aina hiyo na kusubili matamko yake ili kudhibiti matukio jambo ambalo alidai ni kutotekeleza majukumu yao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso