MBIVU NA MBICHI LEO HUKUMU YA RUFAA YA SABAYA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 6 May 2022

MBIVU NA MBICHI LEO HUKUMU YA RUFAA YA SABAYA

 

ARUSHA: Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili wamefikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya rufaa yao kupinga kifungo cha miaka 30 jela.

 

Mbali na Sabaya waomba rufaa wengine ni Sylvester Nyegu na Daniel Mbura ambao wamefika mahakamani kusikiliza rufaa inayosikilizwa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, Sedekia Kisanya wakati wanafikishwa ulinzi ulikuwa umeimarishwa mahakamani hapo.

 

Rufaa hiyo ya jinai namba 129/2021 imeletwa na Sabaya na wenzake hao wakipinga hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

 

Awali Oktoba 15, 2021 Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo aliwahukumu Sabaya na wenzake wawili kifungo cha miaka 30 kila mmoja, baada ya kuwatia hatiani kwa makosa matatu ikiwamo unyang'anyi wa kutumia silaha.

 

Wakati akitoa hukumu hiyo, Hakimu Amworo alisema kwa kuzingatia ushahidi uliotolewa mahakamani, aliridhika washitakiwa hao walimpora Numan Jasin, Bakari Msangi na Ramadhan Rashid.

Chanzo:Mwananchi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso