Madiwani wa halmashauri ya Nsimbo mkoa wa Katavi kwa kauli moja wamesema hawana imani na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Mohamed Ramadhani.
Kauli ya madiwani hao imekuja kufuatia uwepo wa mashamba hekari 846 mali ya halmashauri ambayo yamekodiwa bila kufuata utaratibu na mapato yake hayaeleweki yanapoelekea, huku wananchi wakiendelea kupata mateso kukokana na kukosa maeneo ya kufanyia shughuli za kilimo.
“Tuliosababisha mgogoro ni sisi halmashauri kupitia mkurugenzi wetu huwezi kuwagawia watu heka mojamoja afu eneo nyingine linalobaki useme la kwetu tunasema hatuna imani na mkurugenzi" amesema Michael Kasanga, ambaye ni diwani kata ya Nsimbo.
"Inawezekana we mwenyekiti unatuzunguka mbona mkurugenzi anasema huwa anakaa vikao kujadili eneo hili la eka 846 , huwa anakaa na nani atuambie hapa watu wamepata ulemavu,vifo na wengine wamekimbika yote hii ni sababu ya migogoro ya ardhi watu hawana pakulima". amesema Adam Chalamila, ambaye ni diwani wa kata ya Sitalike.
“Tambueni hatuingili uteuzi wa Rais msitufanye sisi hatujui kwani tumesema hapa kuanzia leo wewe sio mkurugenzi msituyumbishe hapa wala kututisha sisi tunataka kujua na tuna haki ya kujua tumegundua mapungufu na hata tukiamua tutamtoa nje tumjadili nani atatuchalaza viboko hapa" amesema Daniel Itangwa, ambaye ni diwani wa kata ya Ibindi.”
Baada ya madiwani kusimamia kauli kuwa hawana imani na mkurugenzi, kwa hali isiyo ya kawaida alinyanyuka mkurugenzi huyo na kuomba baraza livunjwe na waandike barau ambayo itaelekezwa kwa mkuu wa mkoa ikieleza kuwa hawana imani nae.
“ Kwanza mnavyosema mkurugenzi atoke nje tuendelee na kikao ina maana tuvunje baraza hili tuandike barua kwa mkuu wa mkoa juu ya hiyo hoja ambayo mnaitaka ya kumjadili mkurugenzi.
Mnyukano mkali ulipoendelea kikao kikawa kigumu ilimlazimu mwenyekiti wa halmashauri Halawa Malendeja kusimamisha kikao kwa zaidi ya nusu saa na kutoa fursa kwa wajumbe kujadiliana, na waliporejea walibadilisha ajenda huku msimamo ukiwa ni hatuna imani na Mkurugenzi Mohamed Ramadhani.
“Mnanipa wakati mgumu mimi kama mwenyekiti wa kikao kuamua, mkuu wa wilaya ameshauri na nyinyi wajumbe nawauliza hamjibu kitu mpo kimya ina maana hamjakubaliana na ushauri huo, nawauliza kikao kiendelee hamjibu mimi kama kiongozi najua kabisa hamtaki kuendelea na kikao na mimi siwezi kuendelea bila wajumbe nimeahirisha kwa muda" amesema Halawa Malendeja
Mvutano mkali ulimuinua Jamila Yusuph ambae ni mkuu wa wilya ya Mpanda na kusema wenye mamlaka ndio wenye maamuzi ya kumuondoka kazini mkurugenzi.
No comments:
Post a Comment