Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, limeanza kugawa mipira ya kiume na ya kike (Condom) kwa madiwani wake wote, pamoja na kuwekwa mipira hiyo kwenye maeneo ya huduma za umma zikiwamo ofisi za watendaji wa kata, vijiji, zahanati na sehemu za starehe, ili kuli
Mwenyekiti wa Kamati inayoangazia masuala ya Ukimwi Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Christopher William Ndamo, amesema madiwani na jamii yote lazima washiriki kikamilifu katika mapambano ya ugonjwa huo usiokuwa na dawa wala chanjo.
Wakizungumza kando ya Baraza la Madiwani lililoketi Mjini Mwanhuzi chini ya Mwenyekiti wake, Anthony Philip, baadhi ya madiwani wameshauri kuongezwa kasi ya utoaji elimu kwa jamii, juu ya umuhimu wa kupima afya zao mara kwa mara.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Frank Mganga, amesema kundi la wanawake pamoja na vijana wa kuanzia umri wa miaka 15-29 ndiyo wanaoathirika zaidi na ugonjwa huo, na ametoa rai kwa kila mtu kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo wa Ukimwi.
CHANZO: EATV NEWS
No comments:
Post a Comment